Thursday, May 6, 2010

Maurinho aipa Inter kombe la kwanza




Alikuwa ni Diego Milito aliyewanyamazisha mashabiki wa AS Roma katika dimba la Olimpico na akiwainua mashabiki wa milan waliokuwa wachache uwanjani lakini wengi katika jiji la Milan kushangilia kombe lao la kwanza msimu huu huku wakiyasubiria mengine mawili.

Aliyekuwa na furaha zaidi ni Jose Maurinho ambaye baada ya kuifunga Roma goli moja kwa bila katika mchezo huo wa kombe la ligi la italia, amesema hatimaye ndoto yao ya kwanza imetimia

Inter hivi sasa inapigana kuchukua kombe la ligi kuu ya nchi hiyo pamoja na ligi ya mabingwa barani ulaya.

Ribery kukaa kwa mashabiki fainali ya UEFA


Rufaa ya klabu ya Bayern Munich ya kutaka kupunguziwa kwa adhabu kwa kiungo wake mchezeshaji Frank Ribery imetupiliwa mbali na shirikisho la mpira wa miguu.


Licha ya kutupiliwa mbali rufaa hiyo ya Riery, mwenyekiti wa klabu ya bayern munich, Karl-Heinz Ruminege amesema bado timu yake itaendelea kukata rufaaa hadi waone haki imetendeka kwa kiungo huyo aliyepewa kadi nyekundu katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya dhidi ya Lyon.

Wednesday, May 5, 2010

Mourinho: Nipeni heshima yangu


Kocha mkuu wa InterMilan Jose Maurinho amewataka mashabiki wa InterMilan kumpa heshima yake kutokana na kuisaidia klabu hiyo kufika katika fainali ya mabingwa barani ulaya, kombe la italia na sasa timu hiyo inafukuzia taji la ubingwa wa ligi la nchi hiyo.

Kocha huyo raia wa ureno anaamini timu yake ina nafasi ya kubebwa kikombe cha italia hii leo wakati timu yake itakapokuwa ikivaana na AS Roma katika dimba la olimpico.

akiuzungumzia kikosi chake kabla ya mchezo huo, maurinho anasikitishwa kwa kumkosa kiungo wake mahiri Sjneider pamoja na mlinzi wake mahiri kutoka brazil Lucio lakini bado anaamini atafanya vizuri katika mchezo huo.

Alipoulizwa kuhusiana na nini anachokikumbuka tarehe tano ya mwezi wa tano, kocha hyo mwenye visanga vingi amesema anachokumbuka ni kifo cha Napoleone Bonapatre.

Redknapp: Pressure ipo kwa Man city sio sisi




Kocha mkuu wa klabu ya totenham hotspurs, harry redknapp amesema presha kwa sasa ipo kwa man city na sio kwa klabu yake,.

redknapp moja ya makocha wanaoheshimika sana nchini uingereza ametoa kauli hiyo kabla ya miamba hiyo miwili kuvaana usiku wa leo katika mchezo unaoweza ukaamua ni nani atamaliza katika nafasi ya nne na hatimaye kushiriki katika michuano ya ligi ya mabingwa ulaya.

Kocha huyo wa zamani wa klabu ya portsmouth amesema kuwa wakati ligi inaanza watu wengi waliipigia chapuo man city kumaliza ya nne hivyo anaamini wapinzani wao watashuka dimbani kwa kupania ili watmize adhma yao lakini huku wakihofi timu yake kushinda kwani kama ikishinda leo itakuwa imejihakikishia kabisa kucheza ligi ya mabingwa ulaya msimu ujao.

Wednesday, March 3, 2010

Brazil yaichapa Ireland 2-0 uwanja wa emirates, London


Robinho akishangilia goli la pili aliofunga kiufundi na kumzidi maarifa mmoja kati ya makipa bora duniani Shy Given

Tuesday, March 2, 2010

Capello awaonya wachezaji wake


Kocha mkuu wa timu ya taifa ya uingereza fabio capello amewataka wachezaji wake kusahau matatizo yao binafi yanayowakabili na badala yake waelekeze nguvu zao katika kujiandaa na fainali za dunia.

John Terry na Wayne Bridge wamekuwa katika ugomvi mkubwa wa mapenzi hai iliyomfanya Bridge kujiondoa katika kikosi cha timu ya taifa cha nchi hiyo huku Ashley Cole akiwa ana matatizo na mkewe abaada ya kusaliti ndoa yao

Uingereza inacheza na misri usiku wa leo ktika mchezo wa kujipima nguvu

Monday, February 22, 2010

Drogba kumnyima usingizi kesho maurinho







Timu ya taifa ya soka, Taifa stars imepangwa katika kundi lisilotabirika. Stars itakuwa na kibarua cha kuvaana na Morocco, Algeria pamoja na Afrika ya Kati katika harakati za kuwania tiketi ya kucheza kombe la mataifa ya afrika mwaka 2012 nchini Gabon na Guinea ya Ikweta.

Kwa mujibu wa makundi hayo yaiyotolewa na CAF, kenya pamoja na Uganda ziepangwa pamoja huku zikiwa na upinzani kutoka kwa Angola na nchi nyingine za afrika mashariki zilizopangwa pamoja ni Rwanda na Burundi ambazo zimepangwa na kigogo wa Afrika Magharibi, Ivory Coast.

Monday, February 15, 2010

Norway yazidi kupaa katika olimpiki




Norway imeendelea kuongoza kwa kuchukua medali nyingi katika michezo ya olimpiki ya majira ya baridi yanayoendelea huko vancover nchini Canada. Hadi hivi sasa Norway imejikusanyia medali mia mbili themanini na sita ikifuatiwa na marekani ambayo ina mia mbili hamsini na moja huku ya tatu ikiwa ni umoja wa nchi za kisovieti

Papic aweweseka




Kocha mkuu wa klabu ya yanga ameshindwa kukubali ama kukataa kama matokeo ya timu yake kufungwa na Lupopo goli tatu kwa mbili kuanaweza kuathiri maombi yake ya kutaka kuwa kocha mkuu wa taifa stars.
Kocha huyo amesema hayo baada ya kuulizwa swali na hayqal mushi kuwa anaonaje nafasi yake ya kuwa kocha wa stars baada ya kufungwa na lupopo.
Kwa sasa papic amesema anaelekeza nguvu zake katika mchezo wa marudiano na anaamini anaweza akaivusha mzunguko wa pili.

Monday, February 8, 2010

Yanga yajipanga kuikabili Lupopo




Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania Bara, Dar Young Afrikand wanajiandaa vikali kuikabili mabingwa wa DRC FC Lupopo katika mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa wa afrika utakaochezwa katika dimba la taifa jumamosi hii.

Hivi sasa kikosi cha mabingwa hao kipo katika hali nzuri na hakuna taarifa yoyote ya majeruhi labda baada ya mchezo wa jioni ya leo dhidi ya Mtibwa utakapochezwa.

Mara ya mwisho Yanga kufanya vizuri katika ligi ya mabingwa wa afrika ilikuwa ni mwaka 1999 ambapo ilifika hadi katika hatua ya makundi.

VANESSA PERRONCEL. MCHUCHU ALIYEMCOST JOHN TERRY UNAHODHA ENGLAND.




Binti mwenye asili ya kifaransa. mwanamitindo wa nguo za ndani. yupo addicted na ku-date ma celebrities na wachezaji mpira. baada ya kumcost Terry unahodha sasa anataka kuiuza story yake kwa mamilioni ya pesa kwenye vyombo vya habari.


tumuite husstla? malaya? au ndo maisha. si hatujui ila ni msaliti.


kamsaliti mwanaye Jaydon, kamsaliti mzazi mwenzie Bridge na pia kamsaliti shoga yake Toni Terry mke wa JT.


Yeye na Wayne walikua marafiki wakubwa wa JT na Toni enzi zao za Stamford Bridge. lakini sasa hakuna mwenye ham na mwenzie. tusubiri kwa hamu kuwaona JT na Bridge katika PITCH moja baada ya kuwa on top of BITCH mmoja wa kifaransa ingawa mpaka sasa Wayne ndo anaongoza moja bila baada ya kumzalisha Vanessas. JT yeye goli lake lilikua offside so likakataliwa.

JT, Bridge, Toni, Vanessa na watoto wa JT enzi za Stamford Bridge. hii ilikuwa mwaka 2007.

PLAYERS WHO LOOKS LIKELY TO IMPRESS IN THE WORLD CUP THIS SUMMER.



Samir Handanovic (Slovenia): If Slovenia are to emerge from a group containing England, USA and Algeria, their goalkeeper will need to continue the exceptional form that saw the country concede just four goals in ten games during qualification. Handanovic, 25, is an acrobatic goalkeeper with a good record on penalties and stands at over 6' 5". Current club Udinese may well be braced for interest after the tournament, especially given previous links with some of Europe's top clubs.

GettyImagesAngel Di Maria would love to be the hero in South Africa
Angel Di Maria (Argentina): He'll be competing with the likes of Lionel Messi, Carlos Tevez, Sergio Aguero and most probably Diego Maradona for the headlines about Argentina, but this Benfica winger, who turns 22 shortly, has been in astonishing form this season. Manchester United and Chelsea are both rumoured to be interested in Di Maria as a result and Maradona has tipped him to become a world superstar. With modest opposition in the group stages - Nigeria, South Korea and Greece - and teams likely to focus their efforts on stopping Messi and Co, Di Maria has the chance to establish himself alongside some of his team-mates as a household name.


Yoann Gourcuff (France):


Gourcuff still lacks the star billing of Franck Ribery, Thierry Henry and Nicolas Anelka, but it would be little surprise were he to break through into superstardom this summer. Playing behind the main striker, he has sublime technique, great vision and can score from distance - the attributes that saw Zinedine Zidane etch his name into World Cup legend. He is a key part of Bordeaux's success in France and is currently both Ligue 1 Player of the Year and France Football's French Player of the Year. Raymond Domenech can thank his lucky stars he's not a Scorpio.


Jesus Navas (Spain):


Spain have untold riches in reserve and the likes of Pedro and Sergio Canales will be hoping to make the squad and force their way into the team, but 24-year-old Sevilla winger Navas appears to be better placed to make his mark this summer. He has had serious anxiety problems in the past and suffers panic attacks when spending extended periods of time away from Seville, but he has undergone therapy and now seems to be on top of the problem. Vicente Del Bosque handed Navas his first cap in November and, given his ability to play on either flank, his pace, goal-scoring ability and consistency, he has every chance of international stardom.


Nicklas Bendtner (Denmark):


His performances in the Premier League suggest Bendtner still has work to do to fulfil his potential, but he looks ready to become a real star for his country. He scored goals home and away against Portugal in qualification and was voted Danish Player of the Year and, as Morten Olsen has the side playing well and Denmark have been drawn in a group alongside Netherlands, Japan and Cameroon, Denmark could well enjoy a decent run in the competition with Bendtner supplying the goals.



Mesut Ozil (Germany):


Many have been happy to ignore the old adage that you should never write off the Germans but, beyond the established stars like Miroslav Klose, Michael Ballack and Phillip Lahm, Joachim Loew may have a secret weapon up his sleeve. Ozil, a skilful midfield playmaker who has a history of unfortunate haircuts, turned 21 in October and made his Germany debut only a year ago, but he is already established as a genuine talent for both his club, Werder Bremen, and his country. He's been mooted as a long-term successor for Cesc Fabregas at Arsenal.


Marek Hamsik (Slovakia):


Pavel Nedved, who became a major star after helping Czech Republic reach the final of Euro 96, recently touted Hamsik as his true heir - "he is the player with the characteristics that enable him to play just like me" - and he could play a major part in helping Slovakia make a success of their first ever international tournament. Currently at Napoli and just 22 years old, he, like Nedved, plays in an advanced midfield role or on the left and weighs in with a hefty number of goals.

Oscar Cardozo (Paraguay):


A prolific striker for Benfica in the Portuguese league, 26-year-old Cardozo carries an aerial threat, is comfortable with the ball at his feet and capable of scoring from distance. He has been in Roque Santa Cruz's shadow for his country but, with the Manchester City man continually restricted by injuries, this summer could be his time to shine.


Aaron Lennon (England):


Lennon burst onto the international scene in style at the 2006 World Cup, injecting explosive pace into a lethargic England side from the bench, but suffered a dip in form afterwards. In the last two seasons, though, he has surpassed those early performances and is a major part of Tottenham's Champions League challenge, finally combining his ability to go past defenders with consistently dangerous crosses. However, there are suggestions that a hernia problem could put his World Cup hopes in jeopardy, which would be a major blow for England.


Nilmar (Brazil):


Now 25, Nilmar made his Brazil debut in 2003 and was then recalled by Dunga in 2008 after years in the international wilderness. He was phenomenal from 2007 to 2009 as he returned to first club Internacional after spells with French side Lyon and Corinthians, and that form prompted a big-money move to Villarreal. He has made a positive impact in Spain and now looks the real deal for his country: England fans will remember his headed goal when they faced Brazil in Qatar in November, and he scored five goals in four starts in qualification for the World Cup, including a hat-trick against Chile.
Courtesy of soccernet.com.

Tuesday, February 2, 2010

Hull City yaing´ang'ania Chelsea


klabu ya chelsea imelazimishwa sare ya goli moja kwa moja na klabu ya Hull city hivyo kushindwa kutumia vizuri kiporo chake cha mechi moja alichokuwa nacho.


Hull City ndio waliokuwa wa kwanza kupata goli ambapo katika dk ya 30, Steven Mauyokolo alipiga kichwa safi kilichoenda moja kwa moja katika wavu wa Chelsea.


Goli la kusawazisha la Chelsea lilipatikana katika kipindi cha pili dakika ya 42, kupitia kwa mshambuliaji wake nguli, Didier Drogba ambaye alipiga kiufundi mpira wa adhabu aliomzidi mlinda mlango wa Hull City Boaz Myhill.


Katika hatua nyingine klabu ya Chelsea inatarajia kumpa likizo mlinzi na nahodha wa timu hiyo John Terry ili aweze kushughulikia matatizo yake binafsi yanayomkabili hivi sasa kutokana na kashfa ya kufanya mapenzi na mchumba wa mchezaji mwenzake wa zamani wa Chelsea, Wayne Bridge.

Sunday, January 31, 2010

Misri yafuta machungu ya kukosa kombe la dunia.



Kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Misri, Shawaky Gharib amesema timu yake ilicheza vizuri katika michuano ya kombe la mataifa na hadi ikabeba ubingwa kutokana na kuwa na machungu ya kukosa nafasi ya kucheza kombe la dunia nchini Afrika Kusini.


Kocha huyo ameongeza na kusema kombe la mwaka huu lilikuwa gumu kutokana na timu hiyo kukumbana na mataifa ambayo yatashiriki katika fainali za dunia.


kwa upande wake, mlinda mlango wa Misri Essam El Hadary amesema kikosi chake ndicho kikosi bora katika wakati huu.

Fergie akisifu kikosi chake kwa kuilaza chali Arsenal


kocha mkuu wa klabu ya manchester united, sir alex fergusson amekisifu kikosi chake kwa kuonesha kandanda safi hapo jana na kufanikiwa kuichabanga klabu ya Arsenal goli tatu kwa moja.


Fergie amesifu mbinu aliyoitumia ya kushambulia kwa kushtukiza ambayo iliisaidia kwa kiasi kikubwa timu yake dhidi ya arsenal iliyokuwa imetawala mchezo pamoja na kuishambulia man united mara kwa mara.

Kwa upande wake kocha wa klabu ya Arsenal, Arsen Wenger amekiri kuwa kikosi chake kilicheza mchezo mbovu na makosa ya mchezaji mmoja mmoja yaliigharimu timu yake

Dimba la emirates lipo tayari kwa arsenal na man u



Timu ya taifa ya Togo imefungiwa kushiriki michuano miwili ijayo ya kombe la mataifa ya afrika pamoja na kupigwa faini ya dola elfu hamsini kutokana na kujiondoa katika michuano hiyo inaomalizika leo huko Luanda Angola.


Caf imesema imeamua kutoa adhabu hiyo kutokana na serikali ya Togo kuwashinikiza wachezaji wajiondoe huku wachezaji hao wakitaka kucheza michuano hiyo.


Nayo serikali ya Togo imejibu mapigo na kuishutumu CAF kwa kutoa adhabu hiyo ambapo waziri wa mambo ya ndani ya Togo Paschal Bodjona amekarirwa akishangazwa na uamuzi huo huku akisema Caf haijali maisha ya watu waliopotea maisha wakati timu hiyo iliposhambuliwa na waasi huko Cabinda.


Togo ilishambuliwa na waasi wa Cabinda tarehe nane ya mwezi wa pili ambapo katika shambulio hilo maofisa wawili waliwawa

Terry akumbwa na kashfa ya mapenzi




Nahodha wa timu ya taifa ya uingereza na klabu ya Chelsea ya uingereza, John Terry anakabiliwa na kashfa kubwa ya kumpa mimba mpenzi wa mchezaji mwenzake wa zamani Wayne Bridge.
Inasemekana kuwa Terry alikuwa anatembea na mpenzi huyo wa bridge anayejulikana kwa jina la Vannesa ambaye ni mwanamitindo kutoka nchini Ufaransa. Katika habari za ndani zaidi zinaeleza kuwa Vannesa ametoa mimba hiyo aliyopewa na terry miezi michache iliyopita.

Terry anayepokea kitita cha paund laki moja na sabini kwa wiki alianza mapenzi na vannesa mara baada ya wayne bridge kuuzwa kwa klabu ya Manchester City mwezi wa kwanza mwaka jana

Friday, January 29, 2010

Thursday, January 28, 2010

Misri na Ghana Fainali jpili




Misri imeichapa Algeria iliyomaliza ikiwa na wachezaji nane goli nne kwa buyu katika mchezo wa nusu fainali na kufanikiwa kutinga fainai pamoja na kulipiza kisasi cha kufungwa na mahasimu wake hao wa jadi katika ukanda wa kaskazini mwa Afrika.
Katika mchezo wa mapema, Ghana iliichapa Nigeria goli moja kwa bila na hivyo kufanikiwa kuingia fainali ambapo sasa itacheza na Misri.

Goli la Ghana lilifungwa na Asamoah Gyan ambaye baaada ya filimbi ya mwisho aliangua kilio na alipohojiwa kulikoni alikiri kuwa hakuamini kama kikosi kilichosheheni wachezaji wachanga kama hao kingeweza kufika katika hatua hiyo.

Kama Misri chini ya kocha wake mkuu Hassan Shehata ikichukua ubingwa basi itakuwa imeweka rekodi ya kukibeba kikombe hicho mara saba.

Spotidesk inapochana mawimbi


Murray atinga fainali


Mcheza tennis Andy Murray amefanikiwa kutinga katika hatua ya fainali ya mashindano ya wazi ya Australia baada ya kumshinda Marin Cilic kwa seti 3-6 6-4 6-4 6-2 katika mchezo uliochezwa kwa masaa matatu.


Kwa matokeo hayo Murray atacheza na mshindi kati ya Federer na Tsonga katika fainali ya mashindano ya wazi ya Australia ambapo mchezo wa fainali utachezwa jumapili.

Yanga yatamba kuifunga Majimaji jmosi




Mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara, Yanga wametamba kufanya vizuri katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Majimaji licha ya kuwakosa wachezaji wake muhimu watatu, Mrisho Ngasa na Abdi Kassim kutokana na majeruhi huku Nurdin Bakari akiwa na anakabiliwa na kadi mbili za njano.


Katika hatua nyingine kocha mkuu wa klabu hiyo Kostadin Papic amesema itakuwa ni vigumu kwa timu yake kucheza michezo ya kimataifa ya majaribio nje ya nchi kutokana na kubanwa na muda wa kujiandaa kucheza na klabu ya Lupopo ya kutoka DRC ukiwa mchezo wa ligi ya mabingwa wa Afrika.

Tuesday, January 26, 2010

Sauti za Busara kuanza kusikika trh 11 FEB




Tamasha la saba la sauti za busara linatarajia kuanza kufanyika kuanzia tarehe kumi na moa ya mwezi huu mpaka tarehe kumi na sita katika uwanja wa ngome kongwe uliopo stone town, Zanzibar.


Mwenyekiti wa tamasha hilo ambaye pia ni kiongozi wa bendi ya kilimanjaro, Waziri Ally amesema wana imani kuwa tamasha la mwaka huu litafana kwa kuna wasanii wakubwa kutoka nchi ya zambia, guinea, afrika kusini, marekani na mataifa mengine watatumbuiza.


Kwa upande wake msanii fresh jumbe anayefanya shughuli zake nchini Japan amesema anaimani tamasha la kumi la busara litakuwa bora zaidi kuliko matamasha yote Afrika.

Robinho kuichezea Santos kwa mkopo


klabu ya manchester city ya uingereza imethibitisha kutaka kumtoa kwa mkopo mshambuliaji wake iliyemnunua kwa bei ghal kutoka real madrid Robinho.

kocha mkuu wa City Roberto Mancini amekaririwa akisema kuwa city inafanya mazungumzo ya mwisho mwisho na Santos ili mchezaji huyo ahamie katika klabu yake hiyo ya zamani.

Mancini ameongeza na kusema kuwa anataka kumsaidia robinho aende sehemu ambayo atacheza mara kwa mara ili aweze kupata namba katika kikosi cha timu ya taifa ya brazil kitakachoshiriki katika fainali za kombe la dunia nchini afrika kusini.

Monday, January 25, 2010

Jua alikuchi nusu fainaliAFCON

Wapinzani wa jadi ambao siku zote hawapikiki chungu kimoja wanatarajia kuchuana katika nusu fainali zote mbili za kombe la mataifa ya Afrika. Wapinzani wa kaskazini mwa Afrika Ageria almaarufu kama mbwa mwitu wa jangwani watakabiliana na Mapharao wa Misri ambao watakuwa na mawili kichwani la kwanza kupata ushindi na kutinga fainali huku la pili likiwa la kulipiza kisasi cha kuondoshwa katika fainali za dunia na mbweha hao wanaocheza kwa kasi dakika zote za uwanjani.

Wakati mambo yakiwa hivyo katika nusu fainali hiyo inayokutanisha miamba ya kaskazini, huko magharibi ya afrika kutakuwa na patashika nguo kuchanika kwa kukukutanisha timu ya taifa ya Nigeria almaarufu kama tai mwenye nguvu atakuwa anakabiliana na Ghana nyota weusi mchezo ambao untarajiwa kuwa wa vute ni kuvute kutokana na upinzani uliopo baina ya miamba hiyo ya afrika magharibi

JABULANI WAWA GUMZO AFCON




Mpira utakaotumika katika fainali za kombe la dunia mwaka huu nchini Afrika kusini JABULANI umekuwa gumzo katika fainali za mataifa ya afrika kutokana na kasi yake pindi unapopigwa.

Tayari baadhi ya walinda walango wameshatoa kilio chao kuhusiana na mpira huo wenye jina la kizulu ambalo linamaanisha shangwe kwa lugha ya kiswahili.

Kampuni ya adidas inayotengeneza vifaa vya michezo imekuwa na kawaida ya kutoa aina tofauti ya mipira kila inapofika katika fainali za dunia.




Soka letu lipo enzi za UJIMA!




Hivi ni mimi tu au hata wewe unafikiri hili, mi naona bado soka letu lipo katika UJIMA, embu angalia biashara za karanga, maji ya kunywa, barafu na vitu kede kede vikiuzwa bila mpangilio, hapo bado kitu kibao cha kuonesha matokeo ni vibati tu vimechokaa alafu vya kitambo next time nitakuonesha picha zake ili uweze kuungana na mimi kuwa soka letu lipo enzi za ujima.

Yanga kutumia michezo ya ligi kujiwinda na Lupopo







Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania Bara, Yanga imesema inatumia michezo ya ligi kuu ya Tanzania Bara kama kipimo ama maandalizi ya kujiandaa na mchezo wa mzunguko wa kwanza wa ligi ya mabingwa wa afrika dhidi ya Lupopo kutoka DRC.

Akizungumza katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara kati ya timu yake na Manyema, Afisa Habari wa klabu hiyo Luis Sendeu amesema kuwa licha ya kutumia michezo ya ligi kama maandalizi ya kuivaa lupopo lakini pia inataraji kucheza na klabu ya URA kutoka Uganda pamoja na klabu moja kutoka kenya.

Katika mchezo wa jana, Yanga iliichabanga Manyema goli tatu kwa moja magoli ya Yanga yakifungwa na Mrisho Ngasa huku la Manyema likifungwa na Ally Mohamed.

Saturday, January 23, 2010

Rooney aishusha Arsenal kileleni


Magoli matatu yaliyofungwa na wayne rooney yametosha kuishusha Arsenal kileleni mwa ligi kuu ya Uingereza, minachosubiriwa sasa ni mtanange baina ya wakali hao mh mi naakaa kimya sjui nani atakuwa mbabe

mjomba vipi tena! unahitaji msaada?


Simba ya tafuna maafande uhuru




Klabu ya simba imeendelea na kasi yake ya kusaka ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa timu ya Tz Prisons kwa goli tatu kwa moja katika uwanja wa Uhuru. Magoli ya simba yamefungwa na Mussa Hassan Mgosi mawili dakika ya 2 na 56 huku Nicholas Nyagawa akipachika jengine dakika ya 16 na lile la prisons lilipatikana katika kipindi cha pili dakika ya 62.

Uchaguzi mkuu simba mwezi wa tano


Uchaguzi mkuu wa klabu ya simba unatarajiwa kufanyika tarehe tisa ya mwezi wa tano mwaka huu. Kwa mujibu wa mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa klabu hiyo, Salum Madenge amesema kuwa uchaguzi huo utafanyika tarehe hiyo katika eneo ambalo litapangwa hapo baadae na kamati ya utendaji